MCHAKATO WA UCHAGUZI WA VIONGOZI TAFCA
Mchakato
wa uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA)
unaanza rasmi Septemba 30 mwaka huu kwa uchukuaji fomu kwa wagombea.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA, Ramadhan Mambosasa, fomu
kwa waombaji uongozi zitaanza kutolewa Septemba 30 mwaka huu, na mwisho wa
kuchukua na kurudisha fomu hizo ni Oktoba 4 mwaka huu.
Fomu
hizo zinapatikana ofisi za TAFCA zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar
es Salaam kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 alasiri. Ada ya fomu kwa waombaji
wa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Katibu Msaidizi ni
sh. 200,000.
Nafasi
zilizobaki za Mhazini, mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) na wajumbe wa Kamati ya Utendaji, ada ya fomu ni sh. 100,000.
Uchaguzi wa TAFCA umepangwa kufanyika Novemba 10 mwaka huu.
No comments