MANENO YA UTANGULIZI YA MENEJA WA BIA YA KILIMANJARO PREMIUM LAGER, GEORGE KAVISHE WAKATI WA MAKABIDHIANO YA MABASI KWA KLABU ZA SIMBA NA YANGA KATIKA VIWANJA VYA OFISI ZA KAMPUNI YA BIA TANZANIA SEPTEMBA 21, 2012
Mkurugenzi Mtendaji wa TBL
Viongozi wa TFF,
Viongozi wa Klabu za Simba na Yanga,
Wafanyakazi wa TBL,
Mashabiki
Waandishi wa habari,
Wageni waalikwa
Mabibi na mabwana
Habari za asubuhi.
Kazi yangu ni fupi sana kutoa utangulizi na kufafanua zaidi
ni kwa nini tuko hapa leo. Hii ni hafla muhimu kwetu sisi wadhamini wa klabu za
Simba na Yanga kwani tunatimiza ahadi iliyopo kwenye mkataba na pia
tunahakikisha kuwa timu zetu zinapata usafiri wa uhakika na wenye hadhi.
Mabasi haya yote mawili yana thamani ya shilingi milioni 450
na ni muundo wa Yutong.
Ni ya kisasa kabisa kwani yanabeba abiria 51 akiwemo dereva,
ni imara kwani chasis yake ni 4x2, injini ya mabasi haya ni aina ya 300
HP Cummins, yana retarder ya umeme and
breki aina ya ABS, yana TV mbili za kisasa, muziki wa nguvu wenye spika nane,
milango na mabuti ya kisasa, kioo cha kuangalia nyuma kinachotumia umeme,
jokofu na kiyoyozi.
Tunataka wachezaji wetu wawe na
raha wanaposafiri. Hii ndiyo maana tumeamua kutoa mabasi haya ya kisasa.
Pamoja na kwamba TBL inawajibika
kununua mabasi hayo kwa mujibu wa mkataba, lakini lengo kuu ni kuona kuwa
wachezaji wanakuwa katika mazingira mazuri.
Tunategemea kuwa mtayatunza
mabasi haya vizuri na yatatumika kwa manufaa ya klabu hizi.
Nimefahamishwa kuwa mkiondoka
hapa mtafanya ziara katika matawi yenu mbalimbali kuwaonyesha mashabiki wenu
mabasi haya na hii pia itakuwa fursa nzuri ya mashabiki kukutana na baadhi ya
wachezaji ambao hawajawahi kuwaona.
Napenda kusisitiza kuwa baada ya
kukabidhi mabasi haya yatakuwa ni mali ya klabu hizi kwa hivyo ni jukumu la
kila klabu kutunza vizuri basi lake ili mnaposafiri mujiskie fahari na muendane
na hadhi yenu ya klabu bora na zenye mashabiki wengi Tanzania.
Nawatakia kila la heri hasa
katika ligi kuu na mashindano mengine ya kimataifa ambayo mtashiriki.
Asanteni kwa kunisikiliza.
No comments