KIINGILIO MECHI YA YANGA, SIMBA SH. 5,000
Kiingilio
cha chini kwenye mechi ya Yanga na Simba itakayochezwa Jumatatu (Oktoba 3 mwaka
huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kitakuwa sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya
kijani ambavyo ni 19,648 kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji
60,000.
Mechi
hiyo namba 80 ya Ligi Kuu ya Vodacom itachezwa kwenye uwanja huo kuanzia saa 11
kamili jioni. Watazamaji watakaotaka kuona mechi hiyo wakiwa wameketi kwenye
viti vya rangi ya bluu ambavyo ni 17,045 watalipa sh. 7,000 kwa tiketi moja.
Viingilio
vingine kwenye mechi hiyo ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo
viko 11,897 wakati VIP C inayochukua watazamaji 4,060 itakuwa sh. 15,000. Kwa
upande wa VIP B tiketi ni sh. 20,000 na VIP A yenye watazamaji 748 tu kiingilio
kitakuwa sh. 30,000.
No comments