KAMATI YATANGAZA MCHAKATO WA UCHAGUZI TWFA
![]() |
Msemaji wa TFF, Boniface Wambura |
Kamati
ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) kimetangaza
mchakato wa uchaguzi wa chama hicho ambao unaanza kesho (Septemba 23 mwaka
huu).
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Ombeni Zavala, mchakato utaanza kesho
ambapo fomu zitatolewa ofisi ya TWFA ambayo iko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume,
Dar es Salaam kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 jioni.
Mwisho
wa kuchukua na kurudisha fomu ni Septemba 27 mwaka huu. Nafasi zinazogombewa ni
Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Mhazini, Mjumbe wa Mkutano wa TFF, na
wajumbe watatu wa Kamati ya Utendaji.
Ada
ya fomu kwa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Katibu ni sh. 200,000
wakati nafasi zilizobaki ni sh. 100,000. Uchaguzi wa chama hicho kwa mujibu wa
Kalenda ya Uchaguzi ya Wanachama wa TFF iliyotolewa na Kamati ya Uchaguzi ya
TFF utafanyika Novemba 4 mwaka huu.
No comments