KAMATI YA UCHAGUZI TFF YATUPA RUFANI YA WARUFANI IRFA
![]() |
Msemaji TFF, Boniface Wambura |
Kamati
ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana jana (Septemba
25 mwaka huu) kusikiliza rufani iliyowasilishwa mbele yake na warufani Mussa H.
Mahundi, Abou O. Sillia na Alex Mgongolwa dhidi ya Kamati ya Uchaguzi ya Chama
cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Iringa (IRFA) iliyoomba Kamati ya Uchaguzi ya TFF
kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa IRFA uliofanyika Septemba 8 mwaka huu
Mufindi, Iringa, na kuomba uchaguzi huo ufanyike upya kwa kuendeshwa na
kusimamiwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Deogratias Lyatto, baada ya kupitia
maelezo ya warufani na warufaniwa, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imejiridhisha kuwa
rufani iliyowasilishwa mbele yake na Mahundi, Sillia na Mgongolwa ilikosa sifa
ya kuwa rufani kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF, Ibara ya
8(2), Ibara ya 21(3) na 24(2). Kwa kutozingatia matakwa ya Kanuni za Uchaguzi
za Wanachama wa TFF, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imetupa rufani hiyo.
Kamati
ya Uchaguzi ya TFF imeiagiza Kamati ya Uchaguzi ya IRFA kuchukua hatua dhidi ya
Abuu Changawa kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa
TFF, Ibara ya 28(6) kwa kuingilia mchakato wa uchaguzi wa IRFA siku ya
uchaguzi.
No comments