Grupo Raiz yafanya mambo tamasha la Wiki ya Brazil Dar
Hostess |
Na Mwandishi wetu
BENDI ya Grupo Raiz kutoka Sao, Paulo Brazil
imefanya onyesho la kufuru la tamasha la Wiki ya Brazil lililomalizika jana
Jumamosi kwenye hotel ya Serena.
Grupo Raiz iliweza kupiga nyimbo nyingi maarufu
za miondoko ya Brazil kwa mamia wa mashabiki waliofika kujumuika kuadhimisha
miaka 190 ya Uhuru wan chi hiyo ambayo inaaminika kuwa ni wafalme wa soka
Duniani.
Mashabiki waliofika katika tamasha hilo
lililodhaminiwa na hotel ya Serena na Hennessy kwa kushirikiana na
ubalozi wa nchi hiyo nchini na rais wa mataifa tofauti ambao waliweza
kuona baadhi ya tamaduni za nchi yao.
Mashabiki hao walijumuika stejini kucheza pamoja
na Balozi wa Brazil nchini, Francisco Luz ambaye alikuwa kivutio kikubwa katika
kucheza staili mbali mbali za muziki wa nchi hiyo. Moja ya staili ambayo
imewavutia wengi ni Brazilian Twist iliyochanganyika na staili nyingi mbali
mbali tofauti.
Mbali ya muziki, waliohudhuria tamasha hilo
waliweza kupata vyakula mbali mbali vya asili ya Brazil ambapo viungo vyake
vilitoka nchini Msumbiji na kuvutiwa navyo.
“Tumefuraishwa sana na jinsi mlivyopokea
tamasha la wiki ya Brazil ambayo lilianza Jumatatu iliyopita, ni faraja kwetu
kuona wote tumesheherehea miaka 190 ya uhuru wan chi hii maarufu duniani,”
alisema Alia Hirjee, mkurugenzi wa kampuni ya QWAY International, ambao
ni mawakala pekee wa Moet-Hennessy afrika Mashariki na waratibu wa
tamasha hilo.
Hirjee alisema kuwa waliofika wamefurahia
muziki, chakula na kujua baadhi ya tamaduni za Brazil na kuwaoma wawe mabalozi
wazuri katika kuutangaza utamaduni huo.
No comments