Flaviana Matata ang’ara Wiki ya mitindo ya London
![]() |
Flavian akiwa katika mavazi tofauti |
Imani Makongoro
MWANAMITINDO
maarufu nchini, Flaviana Matata ameendelea kung’ara katika fani hiyo
baada ya kung’ara katika maonyesho ya wiki ya Mavazi ya London, London Fashion Week.
Flaviana
ambaye kwa sasa anaishi nchini Marekani kwa shughuli hizo za maonyesho
mavazi, aliwavutia sana wadau wa maonyesho hayo na kumfanya mwanamuziki
nyota wa kike duniani, Stefani Joanne Angelina Germanotta maarufu kwa jina la Lady Gaga.
Mwanamitindo
huyo aliwasisimua wadau wengi wa mitindo wakiwemo watu maarufu
duniniani na kuendelea kujizolea sifa na kutangaza jina lake na nchi
yake pia.
Flaviana
amekuwa akishiriki katika maonyesho hayo tangu mwaka 2010, hata hivyo
mwaka huu ameonyesha kukomaa zaidi na kuweza kutawala jukwaa hilo.
Maonyesho ya mavazi ya mwaka huu yaliwahusisha wabunifu wengi maarufu wa mitindo ambapo mmoja wapo ni Vivenne Westwood Red Label ambaye anatamba duniani.
Pamoja
na kuwepo kwa mbunifu huyo, mbunifu Philip Treacy naye alifanya mambo
makubwa katika maonyesho hayo yaliyozinduliwa na Lady Gaga.
Flaviana
alipewa heshima kubwa ya kuvaa jaketi la mwanamuziki aliyekuwa mfalme
wa muziki wa aina ya Pop, marehemu Michael Jackson. Pia alivaa mavaz ya
wabunifu maarufu kama Mike Fast na Christopher Raeburn.
Kutokana
na jinsi alivyowenga kutamba katika maonyesho hayo, Flaviana alifanyiwa
mahojiano na gazeti maarufu duniani la Marekani, Wall Street Journal.
Flaviana
ambaye ni Miss Universe Tanzania wa mwaka 2007, aliweza kuipromoti nchi
yake katika maonyesho hayo kama alivyofanya katika mashindano ya Miss
Universe ya mwaka 2007 kwa kushika nafasi ya sita kati ya warembo 10
walioingia fainali. Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications,
Maria Sarungi Tsehai alisema kuwa anajisikia faraja kubwa kuona Flaviana
anaendelea kufanya vyema katika fani hiyo.
Mwisho….
No comments