Edda malkia wa Redd’s Miss Temeke
Na Mwandishi Wetu
Pamoja na kushinda taji hilo, Edda alipata nafasi ya kuingia katika kambi ya Redd's Miss Tanzania na kujinyakulia kitita cha sh.milioni moja na zawadi zenye thamani ya sh. 500,000.
Mrembo huyo ataungana na Flaviana Maeda kutoka Kurasini, kushiriki mashgindano ya taifa (Miss Tanzania), ambaye alijinyakuwa nafasi ya pili na kubeba kitita cha sh. 800,000.
Mrembo Catherine Masumbigana, alishika nafasi ya tatu katika shindano hilo na kuzawadiwa kitita cha sh. 700,000.
Warembo hao watatu wataingia katika kambi ya Redd's Miss Tanzania, ambayo itashirikisha warembo 30, watakaokaa kambini kwa muda wa mwezi mmoja.
Warembo Jesca Haule ambaye alishika nafasi ya nne amejipatia kitita cha sh. 400,000 na nafasi ya tano ilienda kwa Agnes Gudluck ambae amejipatia sh. 300,000.
Washindi wote watatu kila mmoja. atajipatia nguo ya kutokea jioni na viatu, vikiwa na thamani ya kila mmoja sh. 500,000, kutoka katika duka la kisasa la Mariedo Boutique, ambalo litatoa gauni la sh.350,000 na kiatu cha sh 150,000, kwa kila mmoja kwa washindi hao watatu.
Warembo wengine ambao walishiriki kutoka katika vitongoji vya Kurasini, Kigamboni na Chang'ombe, ambao kila mmoja alipata sh. 200,000, ambao ni Angela Gasper, Khadija Kombo, Neema Doreen, Flora Kazungu, Lilian Joseph, Elizabeth Peter, Elizabeth Boniphace, Zulfa Bundala, Mariam Ntakisivya na Esther Albert.
Katika shindano hilo, washehereshaji walikuwa wasanii wanaong’ara katika luninga, Mpoki wa kundi la Komed Original na Steve Nyerere, ambao walionekana kuvunja mbavu za mashabiki waliohudhulia shindano hilo.
Licha ya kuwepo kwa Mpoki na Steven Nyerere, bendi ya muziki Mashujaa ‘Wanakibega’, walitoa burudani ya nguvu chini ya Rais wao Charles Baba.
Taji la Redd's Miss Temeke, linashikiliwa na mrembo Husna Twalib. Warembo wa Miss Temeke walikuwa wakijifua kwa muda wa wiki tatu sasa, chini ya ukufunzi wa Leyla Bhanji, aliyekuwa akisaidiwa na warembo wa miaka ya nyuma wa Miss Temeke akiwemo, Regina Mosha (20020, Hawa Ismail (2003), washiriki wa mwaka jana Joyce Maweda, Mwajabu Juma, Cynthia Kimasha na katika shoo, walifundishwa na Dickson Daud kutoka kundi la THT.
Wadhamini wengine ni City Sports Lounge, Jambo Leo, Mariedo Boutique, Global Publishers, Dodoma Wine, Push Mobile, Mariedo Boutique, 100.5 Times FM, Kitwe General Traders, Fredito Entertainment, katejoshy.blogsport.com na 88.4 Cloud's FM.
No comments