15 WACHUKUA FOMU UCHAGUZI TWFA
![]() |
Lina Kessy |
Wanamichezo
15 wamechukua fomu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye Chama cha Mpira
wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao.
Waliochukua
fomu za kuwania uenyekiti ni Lina Kessy, Isabellah Kapera na Joan Minja. Nafasi
ya Makamu Mwenyekiti imeombwa na Roseleen Kisiwa pekee wakati Katibu Mkuu ni
Amina Karuma na Cecilia Makafu. Macky Mhango pia ni mwombaji pekee aliyeomba
nafasi ya Katibu Msaidizi.
Waombaji
watatu wa nafasi ya mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) ni Furaha Francis, Juliet Mndeme na Zena Chande. Nafasi ya
Mhazini nayo ina mwombaji mmoja tu ambaye ni Rose Msamila.
Sophia
Charles, Rahim Maguza, Telephonia Temba na Jasmin Badar Soud wao wanaomba
nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya chama hicho kwenye uchaguzi huo ambao
utaendeshwa na Kamati ya Uchaguzi ya TWFA chini ya Ombeni Zavalla.
No comments