BODI YA MASHINDANO MISS UTALII TANZANIA YATHIBITISHA MAWAKALA, NAKUTANGAZA NAFASI ZA UWAKALA 2011/2012
Bodi ya Taifa ya mashindano ya Miss Utalii,katika kutekeleza
mkakati wake wa kujiimarisha na kujipanga kwa ajili ya mpango mkakati mpya wa
muda mfupi na muda mrefu wa miaka mitano na wa miaka kumi,imethibitisha
waandaaki wa mashindano hayo katika mikoa na kanda 17, huku ikitangaza
nafasi za wandaaji katika mikoaa na kanda mbalimbali Tanzania bara na Tanzania
Visiwani.
Katika kupitisha makampuni na majina ya waandaaji hao wa
ngazi za mikoa, bodi imezingatia uwezo ,umakini na uwepo wa ofisi na waandaaji
katika wilaya,mikoa na kanda husika. Pia bodi imezingatia kuwa na waandaaji
makini ambao wanaweza kuendana na mfumi mpya wa kitaasisi wa mashindano haya,
mfumo ambao unatoa fulsa ya mgawanyo wa madaraka na uwajibikaji wa pamoja na
kila mmoja katika ngazi yake.
“ Bodi sasa imeamua kujenga taasisi imara ya
kiheshimika na kukubalika kitaifa na kimataifa,ni wakati sahihi sasa kwa
mashindano haya kuchukua nafasi yake ya kuwa shindano bora na kubwa kuliko yote
nchini,Afrika na duniani kwa ujumla, na hili litawezekana tu kwa kuwa na
taasisi imara na makini iliyojengwa na watu na makampuni makini. Wale
waandaaji wababaishaji,mamluki na wahuni sasa Miss utalii Tanzania sio mahala
pake”.
Aidha bodi imewataka wasandaaji wote kukamilisha taratibu na matakwa ya
kanuni na taratibu za mashindano haya,kabla ya kufanya kwa mashindano ya ngazi
zao,ikiwemo kwenda kujitambulisha na kuchukua vibali vya maafisa utamaduni.
Aidha bodi imewaomba maafisa utamaduni wa ngazi zote kutotoa vibadi kwa
waandaaji hao kabla ya kukamilisha taratibu iliwemo kukabidhi zawadi za
washindi na washiriki siku saba kabla ya tarehe za shindano husika.
Mikoa na kanda hizo na majina ya waandaaki katika mabano ni
Arusha,Mara na Kanda ya Kaskazini ( NAman LIMITED COMPANY LTD), Kilimanjaro na
Manyara (NEW VISION PLAN COMPANY LTD),Kagera ( FIOONA FASHION Limited) Mbeya (
WABUNIFU ENTERTAINMENT), katavi ( KATABI COMPANY LIMITED), Dar es
Salaam,Kinondoni,Ilala na Temeke ( Tanzania Film Directors Association
(TAFIDA)) Vyuo Vikuu Dar es Salaam (Eriado Point View) ,Iringa na Kanda ya
Kusini (DELIMA Hotel & Tourism School),Vyuo Vikuu Kanda ya Mashariki ( L.J
MEDIA COMPANY), Mwanza (Fania Beauty and Salon Company).
Mikoa ambayo haijapata waandaaji baada ya maombi ya
waliotuma kutikuwa na sifa, hivyo wenye sifa wajitokeze kuomba kuandaa ni :
Njombe, Pwani, Lindi, Mtwara, Tanga Morogoro, Dodoma, Singida, Shinyanga,
Simiyu, Geita, Tabora, Rukwa, Kigoma, Kanda ya Kati, Kanda ya Mashariki,
Zanzibar, Kanda ya Kusini Nyanda ya Juu, Kanda ya Magharibi, ,Vyuo Vikuu
Kusini,Vyuo Vikuu kaskazini,Vyuo Vikuu Magharibi,Vyuo Vukuu Kati,na Vyuo Vikuu.
Makampuni na watu wanaotaka kuandaa mashindano haya ya Miss
Utalii Tanzania wawasiliane nasi kupitia barua pepe ya missutaliitanzania@gmail.com ,ukurasa wetu wa facebook wa miss tourism/missutalii
tanzania na au ofisi za vyombo mabalimbali za vyombo vya habari. Fainali za
taifa za Miss Utalii Tanzania 2012, sasa zitafanyika siku ya mkesha wa sherehe
za uhuru 8/12/2012 baada ya kuahitishwa kupisha utaratibu na kalenda mpya
ambapo sasa kila mwaka Fainali za taofa zitafanyika siku ya mkesha wa sherehe
za uhuru. Mikoa na kanda zote zinatakiwa kuwa zimekamilisha fainali zake kabla
ya Novemba 15 kila mwaka.
Asante,
Frances Samwel Mwella
Mkitugenzi wa mashinfano ya Ngazi za Wilaya,Mikoa na Kanda
No comments