Bahanunzi, Dida, Chuji waitwa Stars
![]() |
Said Bahanunzi |
KOCHA Mkuu wa timu ya
Taifa, Taifa Stars, Kim Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 21 kwa ajili ya
mechi ya kirafiki itakayochezwa ugenini Agosti 15 mwaka huu.
Akitangaza wachezaji hao
jana kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) alisema
kuwa, wachezaji hao wanatakiwa kuripoti kambini katika Hoteli ya Tansoma Agosti
8 saa 1 jioni kwa ajili ya kuanza mazoezi siku inayofuata.
Kim alisema kuwa,
kikosi hicho cha Taifa Stars kinayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium
Lager, kitakuwa na Makipa watatu ambao ni Deogratias Munishi (Azam), nahodha
Juma Kaseja (Simba) na Mwadini Ali (Azam).
Aliongeza kuwa, Mabeki
ni nahodha msaidizi Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani
(Yanga) na Shomari Kapombe (Simba).
Viungo ni Athuman Idd
‘ Chuji’ (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Moshi (Simba), Mrisho Ngassa
(Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Ramadhan Chombo (Azam), Ramadhan Singano
(Simba), Salum Abubakar (Azam) na Shabani Nditi wa (Mtibwa Sugar).
Wachezaji wanaounda
safu ya ushambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe), ya Congo
DRC, Said Bahanuzi (Yanga), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe),
ya Congo DRC.
Kikosi hicho kipya
kinatarajiwa kusafiri nje ya nchi kucheza mechi ya kirafiki na timu ambayo
haipo ndani ya CECAFA.
No comments