Header Ads

ad

Breaking News

Yanga yatinga robo fainali Kagame, yaipiga El Salam Wau ya Sudan Kusini

Hamis Kiiza
Yanga ya jijini Dar es Salaam, leo imezinduka na kuibuka na ushindi wa mabao 7-1 dhidi ya timu ngeni katika michuano hiyo ya Wa Salaam ya Sudan Kusini, mechi iliyopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Hamis Kiiza mabao matatu, Said Bahanuzi mabao mawili,  Stefano Mwasyika na Nizar Khalfan kila mmoja bao moja.

Sudan Kusini,bao lao lilifungwa dakika ya 88, kupitia kwa Hamisi Bashama. 

Katika mechi ya kwanza iliyopigwa uwanjani hapo kati ya APR ya Rwanda na Atletico ya Burundi, timu hizo zilitoka suluhu.

Kwa matokeo hayo, APR, Atletico na Yanga zimetinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, huku Wa Salaam inayoshiriki kwa mara ya kwanza ikisubiri mechi ya kukamilisha rafitba dhidi ya Atletico, Yanga wao watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya APR.

No comments