Yanga yatangulia nusu fainali Kagame
![]() |
Wachezaji wa Yanga wakishangilia baada ya kushinda kwa penalti |
*Yapita kwa kuichapa Mafunzo kwa penalti 5-4
MABINGWA watetezi wa michuano ya Kombe la
Kagame, Yanga, jana ilikata tiketi ya kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano
hiyo baada ya kuiondosha Mafunzo ya Zanzibar kwa mikwaju ya penalti 5-4, katika
mechi iliyopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Dar es Salaam.
Katika mchezo huo, Yanga walianza kwa
kulisakama lango la wapinzani wao, ambapo dakika ya 23, Hamis Kiiza akiwa
tayari ameotea, alizitikisa nyavu za Mafunzo, lakini tayari mwamuzi Thiesy
Nkurunziza kutoka Burundi alikuwa amepuliza filimbi yake.
Mafunzo walijibu mashambulizi hayo, ambapo
dakika ya 34, Ali Othman Mmanga alliipatia bao timu yake kwa kuunganisha kwa
kichwa mpirawa kona uliopigwa na Ally Juma Hassan.
Kipindi cha pili, Yanga walianza mchezo kwa
kulisakama lango la Mafunzo, ambapo dakika ya 63, Jerryson Tegete aliyeingia
badala ya Rashid Gumbo aliushindwa kutumia vizuri pasi iliyotoka kwa Haruna
Niyonzima kwa kupiga shuti kali lililotoka nje ya lango.
Juhudi za Yanga zilizaa matunda dakika ya 46,
baada ya Said Bahanuzi kuisaizishia timu yake bao kwa kichwa, huku akiwaacha
mabeki wa Mafunzo wakiwa wamesimama bila ya jitihada zozote za kumzuia.
Tegete, jana haikuwa bahati yake kwani dakika
ya 81, alipata nafasi nyingine nzuri, lakini alishindwa kufunga baada ya kupiga
shuti lililokwenda nje ya lango la wapinzani wao.
Baada ya dakika 90 kumalizika, sheria mikwaju
ya penalti ilitumika, ambapo Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa penalti
5-4, na kuiwezesha timu hiyo inayonolewa na Mbelgiji, Tom Seintfiet kutinga
hatua ya nusu fainali.
Katika mechi ya fainali, Yanga watakutana tena
na APR ya Rwanda, ambayo iliiondosha kwenye michuano hiyo URA ya Uganda.
Yanga katika hatua ya makundi ilikutana na APR
na kufanikiwa kuichapa mabao 2-0, hivyo mechi hiyo inatarajiwa kuwa ngumu.
Penalti za Yanga zilifungwa na Bahanuzi, Hamis
Kiiza, Haruna Niyonzima, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Athuman Idd ‘Chuji’,
wakati walioifungia Mafunzo ni Salum Said Shebe, , Mohemmed Abdulrahim, Jaku
Juma Jaku na Said Mussa Shaban alikosa.
Katika mchezo huo, mchezaji wa Mafunzo, Juma
Othman Mmanga alikimbizwa hospitali baada ya kugongana na mchezaji mmoja,
madaktari wa timu zote mbili walimtibu, lakini tatizo lake likaonekana kubwa,
hivyo kumkimbiza hopsitali kwa ajili ya matibabu zaidi.
Yanga SC: Yaw Berko/Ally Mustapa ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua,
Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Stefano Mwasyika/Idrissa
Rashid, Haruna Niyonzima, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na Rashid Gumbo/ Jerryson Tegete.
Mafunzo: Khalid
Mahadhi Hajji, Ismail Khamis Amour/Yusuf Makame Juma, Said Mussa Shaaban, Salum
Said Shebe, Ali Othman Mmanga, Juma Othman Mmanga, Suleiman Kassim ‘Selembe’,
Jaku Juma Jaku, Mohamed Abdulrahim, Wahid Ibrahim na Ally Juma Hassan.
Katika mechi ya kwanza, APR ya
Rwanda ilifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kuilaza URA ya Uganda
mabao 2-1, katika mchezo ulioanza kuchezwa saa nane mchana kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam.
Mabao ya APR yalifungwa na Claude
Iranzi dakika ya tisa na bao la pili lilifungwa dakika ya 34 na Seleman
Ndikumana, wakati URA lao lilifungwa na Robert Ssentongo dakika ya 57.
.![]() |
Raha ya ushindi, kila mmoja kwa mtindo wake akijiburudisha kucheza. |
No comments