yanga yaichapa APR 1-0, kuumana na Azam FC Jumamosi
![]() |
Bahanunzi akiwa amembeba Kiiza |
MABINGWA wa klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati
(Kombe la Kagame), Yanga, jana ilifanikiwa kukata tiketi ya kucheza fainali
baada ya kuilaza APR ya Rwanda bao 1-0, katika mchezo uliopigwa dakika 120
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo, Yanga itakutana na Azam FC ambao
wameiondosha AS Vita katika mechi ya kwanza ya nusu fainali, kwa kuichapa mabao
2-1, Jumamosi.
Katika mchezo huo, APR waliuanza kwa kuliandama
lango la Yanga, ambapo dakika ya 10, Leonel St. Preus alikosa bao baada ya
kupiga shuti kali lililogonga mwamba na
kurudi uwanjani, lakini mabeki wa Yanga wakaokoa mpira huo katika hatari.
Kipa wa Yanga, Ally Mustapha ‘Barthez’, alifanya
kazi kubwa ya kuokoa mpira uliopigwa na St. Preus, aliyewapoteza mabeki wa timu
hiyo na kubaki na kipa, lakini shuti lake liliokolewa.
Shamte Ally, aliyeingia dakika ya 26, alionesha kadi
ya njano baada ya kugusa mpira mara moja dakika ya 40, kwa kumchezea vibaya
mchezaji mmoja wa APR, huku akipigiwa kelele na mashabiki kwamba, atolewe nje.
Dakika ya 66, Said Bahanunzi alifanikiwa kuwatoka
mabeki wa APR na kubaki na kipa Ndoli Claude, lakini shuti lake lilitua
mikononi mwa kipa huyo, ambapo dakika ya 74, Nadir Haroub ‘Cannavaro’,
alishindwa kuifungia timu yake bao baada ya kupiga mpira kichwa, lakini kipa
Ndoli akaondoa kwa mguu na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.
Yanag walipata nafasi nyingine nzuri dakika ya 94,
baada ya David Luhende kupiga shuti kali lililotoka nje ya lango la APR.
Zikishambuliana kwa zamu baada ya kuongezwa dakika
30, Yanga ilipata bao dakika ya 99, lililofungwa na Mganda Hamis Kiiza, ambaye
ni mmoja wa wachezaji wanaosifiwa sana na kocha wa timu hiyo Tom Saintfiet
kuwa, anajituma uwanjani.
Kiiza alipata mpira kutoka kwa Haruna Niyonzima
ambaye aliwapanguwa mabaki wa APR na kummegea pande safi mfungaji wa bao hilo.
Yanga ilipata pigo dakika ya 103, baada ya Godfrey
Taifa kuoneshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje kwa kadi nyekundu na
mwamuzi wa mchezo huo kutoka Kenya, Anthony Ogwayo, baada ya kumtolea lugha
mbaya, kadi ya kwanza alioneshwa kipindi cha kwanza kwa kumchezea vibaya St
Preus.
Yanga: Ally Mustapha ‘Barthez’, Nadir Horoub
‘Cannavaro’, Kelvin Yondan, Haruna Niyonzima, Juma Abdul/Rashid Gumbo, Athuman Idd ‘Chuji’, Oscar Joshua, Hamis
Kiiza, Said Bahanunzi, Godfrey Taita, David Luhende.
APR: Ndoli Claude, Olivier Karekezi, Suleiman
Ndikumana, Jean Mugiraneza, Johnson
Bagoole, Leonel St Preus, Albert Ngabo, Mbuyi Twite, Danny Wagaruka, Tuyizere
ciao
No comments