Wawili wajishindia bajaji Yanga
MASHABIKI
wawili wa klabu ya soka ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, jana walijishidia
zawadi za bajaji katika mchezo wa bahati nasibu wa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi.
Katika
mchezo huo ambao unaendelea, mashabiki 40,000 walituma ujumbe mfupi wa
maandishi na wawili kuibuka vinara.
Mshindi
aliyejipatia bajaj ni Sinyasi Vicent mkazi wa Masasi mkoani Mtwara mwenye miaka
39, ni karani mkoani hapo.
Sinyasi
alipata bajaj hiyo yenye thamani ya sh. milioni 5.5, wakati aliyeondoka na
pikipiki ni Amir Jaffar wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora, pikipiki hiyo ina
thamani ya sh milioni 1.5.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Yanga, Louis
Sendeu, alisema washindi hao walipatikana katika droo iliyochezeshwa jana.
Msimamizi
wa shindano hilo kutoka Push Mobile, Talib Rashid, alisema shindano hilo
linaendelea na mashabiki wa Yanga wanatakiwa kuendelee kushiriki.
Bahati
nasibu hiyo ilisimamiwa na mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha,
Bakari Majid.
“Tangu
tumeanza zoezi hili, tuna siku 90 na kila siku tumekuwa tukipata mshindi mmoja
ambaye hujinyakulia fedha taslimu sh. 50,000, hadi kufikia leo, Yanga wametoa sh.
milioni 4.5,” alisema Rashid.
No comments