Taarifa za Simba
SIMBA SPORTS CLUB
P.O.BOX
15318 | TEL+255 222183330 |FAX +255 222183330 |MSIMBAZI/MCHIKICHI STREET
| DAR ES SALAAM | TANZANIA
| EMAIL simbasportsclub@yahoo.com|
WEBSITE www.simba.co.tz| AFFILIATED TO TFF, DRFA and IDFA
19/07/2012
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MSIBA WA KITAIFA
MWENYEKITI wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, kwa niaba ya
uongozi, wanachama na wapenzi wa klabu hiyo, wanatoa salamu za rambirambi kwa
wananchi wote ambao kwa namna moja au nyingine wameguswa na tukio la ajali ya
boti ya Skaget iliyotokea huko Chumbe, Zanzibar.
Rage amesema katika kipindi hiki ambacho wananchi wa Tanzania wako katika msiba mzito, Simba SC
inapenda kuwapa pole wote waliokumbwa na msiba huu moja kwa moja na inawaombea
kwa Mungu awape moyo wenye subra.
Katika kipindi cha maombolezo, Rage amesema shughuli zote za
sherehe zimesimamishwa ndani ya klabu na bendera za klabu zitapepea nusu
mlingoti katika kipindi hiki cha siku tatu za maombolezo kama
kilivyotangazwa na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk. Ali
Mohamed Shein.
Katika mechi inayofuata ya Kombe la Kagame keshokutwa
Jumamosi dhidi ya AS VITA ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), wachezaji na viongozi wa Simba
watavaa vitambaa vyeusi kama ishara ya kuomboleza
msiba huu mkubwa.
AMIR MAFTAH MRISHO
Mchezaji Amir Maftah ambaye jana aliumia katika pambano
dhidi ya AS Port ya Djibout amefanyiwa vipimo leo na imebanika kwamba ameteguka
(dislocation) kidole chake cha mwisho cha mkono wa kulia.
Kutokana na maumivu hayo, Maftah sasa atakaa nje ya uwanja
kwa muda wa wiki mbili, ikiwa na maana kwamba huenda asicheze kabisa michuano
ya Kombe la Kagame inayoendelea jijini Dar es Salaam.
Uongozi wa Simba na jopo lake la utabibu utamtibia Maftah na
kuhakikisha anarejea uwanjani mapema na akiwa amepona kabisa tatizo lake hilo.
Mkutano na Waandishi
wa Habari
Kesho kutakuwa na mkutano wa waandishi wa habari katika
ofisi za Makao Makuu ya Simba mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam. Mkutano huo utafanyika saa
sita mchana na mzungumzaji mkuu atakuwa Kocha Mkuu wa Simba, Profesa Milovan
Cirkovic.
Mada kuu itakuwa masuala ya kiufundi katika michuano ya
Kagame.
Imetolewa na
Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari
Simba SC
No comments