TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA TASWA
CHAMA
cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kinatoa pole kwa
Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla kutokana na vifo vilivyotokea vya watu
zaidi 60 baada ya kuzama kwa meli ya Mv Skagit juzi eneo la kisiwa cha Chumbe,Zanzibar.
TASWA
inaungana na Watanzania katika kipindi hiki kigumu, huku tukiwaombea
waliofariki Mwenyezi Mungu ahifadhi roho zao mahali pema na wale majeruhi awape
nguvu wapone haraka waweze kuendelea na shughuli zao za ujenzi wa Taifa.
Tunaziomba
familia zilizopoteza ndugu zao ziwe na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu na
waamini kwamba huo ni msiba wetu sote na si wao peke yao.
TASWA
inaamini wapo wanamichezo waliopoteza maisha kwenye meli hiyo na pia wapo
wanamichezo waliopoteza ndugu na jamaa zao, wote tunawapa pole na wawe na moyo
wa subira.
(B)
MKUTANO
MKUU WA MWAKA
Kamati ya Utendaji ya TASWA inatarajia
kukutana hivi karibuni pamoja na mambo mengine kujadili masuala mbalimbali ya
maendeleo ya chama hicho ikiwemo kupanga tarehe ya Mkutano Mkuu wa mwaka.
Awali sekretarieti ya TASWA ilipendekeza
mkutano huo uwe mwanzoni mwa Agosti, lakini ili kuepuka kuingiliana na mwezi
mtukufu wa Ramadhan mkutano huo sasa utafanyika mwishoni mwa Agosti katika
tarehe na ukumbi ambao utapangwa na Kamati ya Utendaji.
Nawasilisha.
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
20/07/2012
No comments