Header Ads

ad

Breaking News

Swahili Multchoice ya futurisha wandishi wa habari

 

NA MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya Maultchoice na wasambazaji wa DSTV nchini imewataka wadau mbalimbali kujiunga na mtandao huo kwa ajili ya kujipatia Michezo na burudani.
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana, na Meneja Mahusiano Mkuu wa Multchoice Tanzania, Babra Kambogi, wakati wa hafla fupi ya kufuturisha  waandishi wa habari  za michezo iliyoandaliwa na kampuni hiyo.
Alisema DSTV imekuwa ikiwaletea wadau wa michezo na burudani mambo mazuri kila kukicha hivyo ni fursa nzuri kwa kila mtu kujipatia vifurushi mbalimbali vinavyolingana na fedha zao.
Babra alisema DSTV imezindua chaneli nane ambazo zitahusika moja kwa moja na kuonyesha zawadi za michezo ya Olimpic iliyoanza juzi nchini Uingereza.
Vilevile alisema walitenga chanel mbili maalumu za Kiswahili zilizokuwa zikitumika kurusha matangazo ya mashindando ya Kombe la Kagame yaliyomalizi jana jijini
ambapo watangazaji wake walikuwa Watanzani.
Babra alisema huo ni muendelezo wa kampuni hiyo katika kuwafikishia wadau wake michezo, burudani  na tamthiria mbalimbali popote walipo. www.fullshangwe.blospot.com
Baadhi ya Waandishi habari kutoka vyombo mbalimbali nchini waliohudhuria hafla hiyo wakijisevia Futari.
Mkurugenzi wa Jambo Concept Benny Kisaka.
Huku wengine wakiendelea kubadilishana mawazo.
Waandishi wa habari wakienjoy futari iliyoandaliwa na kampuni ya Multichoice Tanzania.
Katikati ni Ankal Issa Michuzi sambamba na Mwenyekiti wa TASWA Juma Pinto (kulia).

No comments