Simba yanogeshwa kwa jezi mpyaa kuonekana kesho dhidi ya Azam FC
SIMBA SPORTS CLUB
P.O.BOX 15318 | TEL+255 222183330 |FAX +255 222183330
|MSIMBAZI/MCHIKICHI STREET | DAR ES SALAAM | TANZANIA | EMAIL simbasportsclub@yahoo.com|WEBSITE
www.simba.co.tz| AFFILIATED TO TFF, DRFA and IDFA
23/07/2012
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Shukrani kwa Familia
ya Al Ruwahi
KLABU ya soka ya Simba jana imepokea msaada wa jezi, raba,
viatu vya kuchezea mpira, mabegi na suti za michezo (tracksuit) – vyote vya
kisasa kabisa, kutoka kwa familia ya Al Ruwahi. Msaada huo umetolewa kwa
mapenzi mema ambayo familia hiyo inayo kwa klabu.
Ikumbukwe kwamba mahusiano baina ya familia ya Al Ruwahi
(Ruwehi) na Simba yamedumu kwa zaidi ya miaka 30 sasa. Takribani miaka 30
iliyopita, familia hiihii ilitoa zawadi ya basi (Nissan Coaster) kwa Simba na
kuifanya klabu yetu kuwa ya kwanza nchini kumiliki basi lake yenyewe.
Msaada huo wa sasa kwa Simba una thamani ya Sh milioni 18
kwa ujumla wake na Simba sasa itavaa jezi hizo katika pambano lake la kesho
dhidi ya Azam katika michuano ya Kombe la Kagame.
Klabu ya soka ya Simba inatumia nafasi hii kuwakaribisha
wapenzi na wanachama wake kujitokeza kuisaidia klabu kwa namna yoyote ile, kama
ilivyofanya familia hii ya Al Ruwahi, ili kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya klabu.
Simba ni ya kila mmoja na haina mwenyewe. Umoja na
mshikamano baina ya viongozi, wadhamini, wapenzi na wanachama wake, ndiyo
utakaoifanya izidi kuwa bora hapa nchini na nje ya mipaka ya taifa letu.
Kombe la Kagame
HALI za wachezaji waliopo katika kambi Hoteli ya Vina
iliyopo Mabibo jijini Dar es Salaam inaendelea vizuri. Majeruhi ni mmoja tu,
Amir Maftah na Abdallah Juma amefanyiwa vipimo jana na majibu yake yanatolewa
baadaye leo.
Kwa mujibu wa CECAFA, wachezaji wote waliokuwa na kadi moja
ya njano kwenye hatua ya makundi wamefutiwa kadi zao na hivyo Simba itaingia
uwanjani kesho Jumanne kwenye pambano dhidi ya Azam ikiwa haina mchezaji mwenye
adhabu.
Simba imesifiwa na CECAFA kuwa ni miongoni mwa timu zenye
nidhamu nzuri kwenye michuano ya Kagame mwaka huu, mfano ukitolewa kwenye
pambano lake dhidi ya AS VITA ya DR Congo, ambapo hakukuwapo na kadi yoyote
iliyotolewa mechi nzima.
Wenu
Ezekiel Kamwaga
Ofisa Habari
Simba SC
![]() |
Kikosi cha Simba |
No comments