Header Ads

ad

Breaking News

Mbelgiji wa Yanga apanga kukifumua kikosi chake


Kikosi cha Yanga

KOCHA Mkuu wa Yanga, Tom Saintfiet, amesema kuwa,  ili kuwa na matokeo bora kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara, itabidi kufanya baadhi ya mabadiliko kwenye kikosi chake.

Akizungumza na SuperStar jijini Dar es Salaam, Saintfiet aliseama kuwa, kikosi chake kipo imara, lakini yapo mambo ya kufanyia marekebisho ili kupata mafanikio kwenye michuano mbalimbali, ikiwemo ligi ya Bara.

“Tupo kwenye hatua nzuri ya maandalizi ya ligi, lakini jambo linaloonekana kwa sasa, ni lazima kuwa na mabadiliko katika timu.

“Kama unavyojua, ili kuwepo na manufaa na matokeo bora, ni lazima tuwe na mabadiliko katika baadhi ya mambo katika kikosi chetu.

“Hili ni jambo ambalo lipo mikoni mwangu, hivyo sina budi kufanya mambo ya aina hiyo kwa nanufaa ya Yanga.

“Kama tukifanikiwa kutwaa Kombe la Kagame, ni wazi kuwa, kazi kubwa itakayokuwa imebakia ni ligi tu,” alisema Saintfiet raia wa Ubelgiji.

Kocha huyo kwa sasa anakabiliwa na kibarua kigumu cha kuhakikisha kwamba, wanatwaa ubingwa wa Bara ili kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Afrika.

No comments