MANJI NA JESHI LAKE LA MIAMVULI WAWAPA SUMU WACHEZAJI YANGA KUUA WAZENJI KESHO
MWENYEKITI
wa klabu ya Yanga, Yussuf Manji leo ametembelea tena makao makuu ya
klabu hiyo mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam na kuzungumza na
wachezaji.
Manji
alifika klabuni hapo akiwa ameongozana na makamu wake, Clement Sanga,
wajumbe wa kamati ya utendaji, Abdalla Bin Kleb na Mussa Katabalo pamoja
na aliyekuwa makamu mwenyekiti wa kamati ya usajili, Seif Ahmed.
Viongozi
hao walikutana na wachezaji kwa saa kadhaa na kuzungumza nao mambo
mbalimbali kwa lengo la kuwaweka sawa kabla ya mechi yao ya robo fainali
ya michuano ya Kombe la Kagame dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar.
Yanga
inatarajiwa kushuka dimbani leo kucheza na Mafunzo katika mechi ya pili
ya robo fainali itakayoanza saa 10 jioni. Katika mechi ya awali, URA ya
Uganda itavaana na APR ya Rwanda.
Katika
kikao hicho cha faragha, inasemekana kuwa Manji na viongozi wenzake
waliwataka wachezaji kutambua vyema jukumu lililo mbele yao na kuongeza
jitihada ili waweze kufika mbali zaidi.
Alisema
mechi hiyo ni muhimu kwao kwa vile iwapo wataishinda Mafunzo watafuzu
kucheza nusu fainali na hivyo kujiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya
kutwaa ubingwa.
No comments