MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AWAFARIJI WAFIWA NA WAHANGA WA AJALI YA MELI YA SKIGET ZANZIBAR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, wakati alipofika Ikulu mjini
Zanzibar leo Julai 19, 2012 kwa ajili ya kumpa pole kuhusu ajali ya
Meli ya Skiget mali ya Kampuni ya seagull, iliyotokea
jana eneo la Kisiwa cha Chumbe. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akimsikiliza mmoja kati ya vijana walionusulika katika ajali ya
Meli ya Skiget, Kitwana Makame Ali (24) mkazi wa Unguja, wakati
alipotembelea katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Unguja, leo Julai
19, 2012 kuwafariji wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo baada
ya kuokolewa katika ajali hiyo iliyotokea jana eneo la Kisiwa cha
Chumbe. Kulia ni Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia
Muungano, Samia Suluhu Hassan.Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, akizungumza na mgonjwa aliyenusulika katika ajali ya Meli ya
Skiget, Hamisa Akida (45)mkazi wa Ununio mjini Bagamoyo, wakati
alipotembelea katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Unguja, leo Julai
19, 2012 kuwafariji wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo baada
ya kuokolewa katika ajali hiyo iliyotokea jana eneo la Kisiwa cha
Chumbe. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
No comments