Header Ads

ad

Breaking News

Simba yaitupa Es Setif Kombe la Shirikisho

Emmanuel Okwi

Simba ya Tanzania imedhihirisha uwezo wake baada ya kufuzu kuingia kwenye makundi kwenye mchezo uliofanyika huko Setif Algeria baada ya kufungwa magoli 3-1 na timu ya ES Setif usiku huu.

Katika mechi ya kwanza iliyopigwa nyumbani kwenye kitalu cha Taifa jijini Dar es salaam wiki mbili zilizopita, Simba ilishinda mabao 2-0, kwa sheria ya goli la ugenini simba imesonga mbele katika michuano hiyo.
Katika mechi hiyo, Simba walipata pigo mapema dakika ya 12, baada ya beki wake wa kati Juma Nyoso, kutolewa nje kwa kuoneshwa kadi nyekundu.
Es Setif  walipata bao la kwanza dakika ya 34 na kuongeza la pili  dakika ya 47, kabla ya kumalizia bao lao la tatu dakika ya 52. 
 
Ushindi wa Simba uliowapeleka mbele kwenye michuano hiyo lilifungwa dakika ya 91, kupitia kwa mchezaji wa kimataifa kutoka Uganda, Emmanuel Okwi.
 
Okwi aliyepokea mpira na kuwatoka mabeki wa Es Setif, alipiga shuti kali lililokwenda moja kwa moja wavuni.
 
Hongera wawakilishi wetu katika michuano ya kimataifa.

No comments