Majonzi kwa watanzania, Kanumba hatunaye tena!
Mwigizaji maarufu wa filamu nchini Steven Kanumba, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo, habari zinasema mwili wa mwigizaji huyo umepelekwa katika hospitali ya Taifa ya Muhibili ili kuhifadhiwa.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Charles Kenyela, amethibitisha juu ya kifo cha mwigizaji huyo na kuongeza kwamba, sababu za kifo chake bado zinafanyiwa uchunguzi lakini taarifa za mwazo ambazo polisi wamezipata zinasema Kanumba alikuwa na mpenzi wake chumbani na kulitokea kutokuelewana kati yao na kusababisha ugomvi mpaka kifo chake.

KAPSHENI: Mwigizaji wa filamu nchini, Steven Nyerere (katikati), akizungumza na waandishi wa habari katika msiba wa nguli wa filamu nchini Steven Kanumba aliyefariki usiku wa kuamkia leo.
Baadhi ya wasanii wakiomboleza nyumbani kwa marehemu Kanumba. |
Baadfhi ya waigizaji wakijadili jambo. |
MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU STEVEN KANUMBA AMEN
No comments