Makali ya Vumilia & K-Mondo Sound kuonekana Zhong Hua Garden
Vumilia Mwaipopo
MWANAMUZIKI wa muziki wa kizazi kipya anayeimba miondoko ya Zouk, Vumilia Abraham akiwa na bendi yake ya K-Mondo Sound, wameingia mkataba wa kutumbuiza katika ukumbi wa Zhong Hua Garden uliopo Victoria jijini Dar es Salaam.
Vumilia ambaye kwa sasa anatamba kibao chake cha Nasepa, amechukua nafasi iliyoachwa wazi na mwanamuziki, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, ambaye alikuwa akitumbuiza hapo kila Jumamosi.
Tangu kuondoka kwa Jaydee, Jumamosi lilikuwa likiporomoshwa disko.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, kiongozi wa K-Mondo Sound Richard Mangustino, alisema mbali na onesho hili pia, wamemnasa mwimbaji mpya aliyewahi kutamba na kibao cha Dokta, Salum Kumpeneka.
Kuhusu onesho, Zhong Hua Garden, alisema ni uamuzi wa kuwasogezea zaidi mashabiki wao burudani baada ya kupiga maeneo ya mbezi kwa muda mrefu zaidi.
“Mashabiki waliokuwa wakilalamika kuwa, Mbezi mbali sasa watawpata uhondo wa nyimbo zetu, kama inavyojulikana bendi yetu inapiga muziki wa aina zote, hivyo ni bora waje kushuhudia makali yetu, shoo itakuwa maalum, na zitapigwa nyimbo zote kali kutoka K-Mondo pamoja na copy za nje,” alisema.
Mangustino alisema K-Mondo ni taratibu haina haraka, na imekuja kuonesha wapenzi wa burudani nini maana ya burudani.
Alisema bendi yao itaendelea kutumbuiza Triz Motel kila Ijumaa, na Jumapili itakuwa Giraffe Hotel, Mbezi Beach.
Kiongozi huyo aliwataka wakazi wa Oysterbay kukaa mkao wa kula, kwani wanatarajia kuwapa raha kila Jumatano, mambo yakikamilika.
K-Mondo kwa sasa inatamba na nyimbo za Njiwa, Magambo, Nelly, Nasepa, Tatizo Umasikini, Utanikumbuka na Sheria.

No comments